Efe 4
4
Umoja katika Mwili wa Kristo
1 #
Kol 1:10
Kwa hiyo nawasihi, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa; 2#Kol 3:12-13kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo; 3#Kol 3:14,15na kujitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani. 4#Rum 12:5Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu.
5 #
Yn 10:16; 1 Kor 8:6 Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. 6#1 Kor 12:6Mungu mmoja, naye ni Baba wa wote, aliye juu ya yote na katika yote na ndani ya yote. 7#Rum 12:3,6; 1 Kor 12:11Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo. 8#Zab 68:18; Kol 2:15Hivyo husema,
Alipopaa juu aliteka mateka,
Akawapa wanadamu vipawa.
9 #
Yn 3:13
Basi neno hilo, Alipaa, maana yake nini kama siyo kusema kwamba yeye naye alishuka mpaka pande zilizo chini za nchi? 10Naye aliyeshuka ndiye yeye aliyepaa juu sana kupita mbingu zote, ili avijaze vitu vyote. 11#1 Kor 12:28; Mdo 21:8Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu; 12#1 Pet 2:5; 2 Tim 3:17kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, hata kazi ya huduma itendeke, hata mwili wa Kristo ujengwe; 13#Kol 1:28hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, hata kuwa mtu mkamilifu, hata kufika kwenye cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo; 14#1 Kor 14:20; Ebr 13:9ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. 15#Efe 1:22; 5:23; Kol 1:18Lakini tuishike kweli katika upendo na kukua hata tumfikie yeye katika yote, yeye aliye kichwa, Kristo. 16#Kol 2:19Katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa kwa msaada wa kila kiungo, kwa kadiri ya utendaji wa kila sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.
Maisha ya Zamani na Mapya
17 #
Rum 1:21; Kol 2:4,6 Basi nasema neno hili, tena nashuhudia katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waenendavyo, katika ubatili wa nia zao; 18#Efe 2:12; Kol 1:21; 1 Pet 1:14ambao; akili zao zimetiwa giza, nao wamefarikishwa na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo ndani yao, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yao; 19#Kol 3:5ambao wakiisha kufa ganzi wanajitia katika mambo ya ufisadi wapate kufanyiza kila namna ya uchafu kwa kutamani. 20Bali ninyi, sivyo mlivyojifunza Kristo; 21ikiwa mlimsikia mkafundishwa katika yeye, kama kweli ilivyo katika Yesu, 22#Kol 3:9; Rum 8:13; Gal 6:8mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; 23#Rum 12:2na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; 24#Mwa 1:26; Kol 3:10mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.
Amri za Maisha Mapya
25 #
Zek 8:16; Kol 3:8 Basi uvueni uongo, mkaseme kweli kila mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, kila mmoja kiungo cha wenzake. 26#Zab 4:4; Yak 1:19,20Mwe na hasira, ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka; 27wala msimpe Ibilisi nafasi. 28#1 The 4:11Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo nzuri kwa mikono yake mwenyewe, apate kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji. 29#Efe 5:4; Kol 3:16,17; 4:6Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia. 30#Efe 1:13; Isa 63:10Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi. 31#Kol 3:8Uchungu wote na ghadhabu na hasira na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na kila namna ya ubaya; 32#Kol 3:13; Mt 6:14; 18:22-35tena iweni wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkasameheane kama na Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.
Iliyochaguliwa sasa
Efe 4: SUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.