Mhubiri 4:9-10
Mhubiri 4:9-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Ni afadhali kuwa wawili kuliko mtu kuwa peke yake. Kwa sababu wawili watapata tuzo la kazi yao. Ikijatokea mmoja akaanguka, huyo mwenzake atamwinua. Lakini ole wake aliye peke yake akianguka! Huyo hatakuwa na mtu wa kumwinua!
Mhubiri 4:9-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Kwa sababu wana tuzo njema kwa kazi yao. Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!
Mhubiri 4:9-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja; Maana wapata ijara njema kwa kazi yao. Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!