Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mhu 4

4
1Kisha nikarudi na kuona madhalimu yote yanayotendeka chini ya jua; na tazama, machozi yao waliodhulumiwa, ambao walikuwa hawana mfariji; na upande wa wale waliowadhulumu kulikuwa na uwezo, walakini wale walikuwa hawana mfariji. 2#Ayu 3:17; Mhu 2:17Kwa hiyo nikawasifu wafu waliokwisha kufa kuliko wenye uhai walio hai bado; 3#Ayu 3:11; Mhu 6:3; Mt 24:19; Lk 23:29naam, zaidi ya hao wote nikamwita heri yeye asiyekuwako bado, ambaye hakuyaona mabaya yanayotendeka chini ya jua.
4Tena nikafikiri amali zote, na kila kazi ya ustadi, ya kwamba inatoka katika mtu kupingana na mwenzake. Hayo nayo ni ubatili na kujilisha upepo.
5 # Mit 6:10 Mpumbavu huikunja mikono yake,
Naye hula chakula chake mwenyewe;
6Heri konzi moja pamoja na utulivu,
Kuliko konzi mbili pamoja na taabu;
na kujilisha upepo.
7Kisha nikarudi tena, na kuona ubatili chini ya jua. 8#Mit 27:20; Mhu 1:8; Hab 2:5,6; 1 Yoh 2:16; Zab 39:6; Lk 12:20Kuna mtu aliye peke yake, wala hana wa pili wake; naam, hana mwana wala ndugu; hata hivyo amali yake haina mwisho, wala macho yake hayashibi utajiri. Basi asema, Ni kwa ajili ya nani nafanya kazi, na kujinyima nafsi yangu mema? Hayo nayo ni ubatili, naam, ni taabu kubwa.
Thamani ya kuwa na Rafiki
9Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja;
Maana wapata ijara njema kwa kazi yao.
10Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua! 11Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kuona moto? 12Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watampinga; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.
13Heri kijana maskini mwenye hekima
Kuliko mfalme mzee mpumbavu.
ambaye hajui tena kupokea maonyo. 14Kwa maana kutoka gerezani alikuja kumiliki; naam, hata katika ufalme wake alizaliwa hali ya umaskini. 15Nikawaona wote walio hai waendao chini ya jua, ya kwamba walishikamana na huyo kijana, huyo wa pili aliyesimama badala ya yule. 16Hawakuwa na kikomo hao watu wote, hao wote ambao alikuwa juu yao; lakini hata hivyo wale wafuatao baada yake hawatamfurahia. Hakika hayo pia ni ubatili, na kujilisha upepo.

Iliyochaguliwa sasa

Mhu 4: SUV

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha