Kumbukumbu la Sheria 12:8-10
Kumbukumbu la Sheria 12:8-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Msifanye kwa kufuata mambo yote tuyafanyayo hapa leo, kila mtu kama aonavyo vema machoni pake; kwani hamjafikilia bado katika raha na urithi akupao BWANA, Mungu wako. Lakini mtakapovuka Yordani na kukaa katika nchi anayowarithisha BWANA, Mungu wenu, akawapeni raha, akiwaokoa na adui zenu pande zote, mkakaa salama
Kumbukumbu la Sheria 12:8-10 Biblia Habari Njema (BHN)
“Msifanye kama tunavyofanya sasa, kila mtu kama apendavyo mwenyewe; kwa sababu bado hamjaingia mahali pa kupumzikia na katika urithi anaowapeni Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Lakini mtakapovuka mto Yordani na kuishi katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawapa mu irithi, na atakapowapatia pumziko msisumbuliwe na adui zenu wote watakaowazunguka ili muishi salama
Kumbukumbu la Sheria 12:8-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Msifanye kwa kufuata mambo yote tuyafanyayo hapa leo, kila mtu kama apendavyo; kwani hamjafikia bado katika raha na urithi akupao BWANA, Mungu wako. Lakini mtakapovuka Yordani na kukaa katika nchi anayowarithisha BWANA, Mungu wenu, akawapeni raha, akiwaokoa na adui zenu pande zote, mkakaa salama
Kumbukumbu la Sheria 12:8-10 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Msifanye kama tunavyofanya hapa leo, kila mtu anavyopenda mwenyewe, kwa kuwa bado hamjafikia mahali pa mapumziko na urithi ambao BWANA Mungu wenu anawapa. Lakini mtavuka Yordani na kuishi katika nchi BWANA Mungu wenu anayowapa kama urithi, naye atawapa pumziko kutokana na adui zenu wote wanaowazunguka ili ninyi mpate kuishi kwa salama.