2 Samueli 22:31-37
2 Samueli 22:31-37 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mungu njia yake ni kamilifu; Ahadi ya BWANA imehakikishwa; Yeye ndiye ngao yao Wote wanaomkimbilia. Maana ni nani aliye Mungu, ila BWANA? Ni nani aliye mwamba, ila Mungu wetu? Mungu ndiye ngome yangu yenye nguvu; Naye huwaongoza wakamilifu katika njia yake. Huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu; Na kunisimamisha mahali pangu pa juu. Ananifundisha mikono yangu vita; Hata mikono yangu yaupinda upinde wa shaba. Nawe umenipa ngao ya wokovu wako; Na unyenyekevu wako umenikuza. Umezifanyizia nafasi hatua zangu, Wala miguu yangu haikuteleza.
2 Samueli 22:31-37 Biblia Habari Njema (BHN)
Anachofanya Mungu hakina dosari! Ahadi ya Mwenyezi-Mungu ni ya kuaminika; yeye ni ngao kwa wote wanaomkimbilia. “Nani aliye Mungu isipokuwa Mwenyezi-Mungu? Nani aliye mwamba wa usalama ila Mungu wetu? Mungu huyu ndiye kimbilio langu imara, na ameifanya njia yangu iwe salama. Ameiimarisha miguu yangu kama ya paa, na kuniweka salama juu ya vilele. Hunifunza kupigana vita, mikono yangu iweze kuvuta upinde wa shaba. Umenipa ngao yako ya kuniokoa; msaada wako umenifanya mkuu. Umenirahisishia njia yangu; wala miguu yangu haikuteleza.
2 Samueli 22:31-37 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mungu njia yake ni kamilifu; Ahadi ya BWANA imehakikishwa; Yeye ndiye ngao yao Wote wanaomkimbilia. Maana ni nani aliye Mungu, ila BWANA? Ni nani aliye mwamba, ila Mungu wetu? Mungu ndiye ngome yangu yenye nguvu; Naye huwaongoza wakamilifu katika njia yake. Huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu; Na kunisimamisha mahali pangu pa juu. Ananifundisha mikono yangu vita; Hata mikono yangu inaupanda upinde wa shaba. Nawe umenipa ngao ya wokovu wako; Na unyenyekevu wako umenikuza. Umezifanyia nafasi hatua zangu, Wala miguu yangu haikuteleza.
2 Samueli 22:31-37 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu; neno la BWANA halina dosari. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake. Kwa maana ni nani aliye Mungu zaidi ya BWANA? Ni nani aliye Mwamba isipokuwa Mungu wetu? Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu. Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu, huniwezesha kusimama mahali palipo juu. Huifundisha mikono yangu kupigana vita; mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba. Hunipa ngao yako ya ushindi, unajishusha chini ili kuniinua. Huyapanua mapito yangu, ili miguu yangu isiteleze.