2 Samueli 22:1-7
2 Samueli 22:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Daudi alimwimbia Mwenyezi-Mungu maneno ya wimbo ufuatao siku ile Mwenyezi-Mungu alipomkomboa mikononi mwa adui zake, na mkononi mwa Shauli. Alisema, “Mwenyezi-Mungu ni mwamba wangu, ngome yangu, na mkombozi wangu. Mungu wangu, mwamba wangu, ninayemkimbilia usalama; ngao yangu, nguvu ya wokovu wangu, ngome yangu na kimbilio langu. Mwokozi wangu; unaniokoa kutoka kwa watu wakatili. Namwita Mwenyezi-Mungu astahiliye sifa anisaidie, nami naokolewa kutoka kwa adui zangu. “Maana mawimbi ya kifo yalinizingira, mafuriko ya maangamizi yalinivamia; kamba za kuzimu zilinizinga, mitego ya kifo ilinikabili. “Katika taabu yangu, nilimwita Mwenyezi-Mungu; nilimwita Mungu wangu. Toka hekaluni mwake aliisikia sauti yangu, kilio changu kilimfikia masikioni mwake.
2 Samueli 22:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi Daudi akamwambia BWANA maneno ya wimbo huu, siku ile BWANA alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na mkononi mwa Sauli; akasema, BWANA ndiye jabali langu, na ngome yangu, na mwokozi wangu, Mungu wa mwamba wangu, nitamwamini yeye; Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, mnara wangu, na kimbilio langu; Mwokozi wangu, waniokoa na jeuri. Nitamwita BWANA astahiliye kusifiwa; Hivyo nitaokoka na adui zangu. Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu. Kamba za kuzimu zilinizunguka; Mitego ya mauti ikanikabili. Katika shida yangu nilimwita BWANA, Naam, nikamlalamikia Mungu wangu; Naye akaisikia sauti yangu hekaluni mwake, Kilio changu kikaingia masikioni mwake.
2 Samueli 22:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi Daudi akamwambia BWANA maneno ya wimbo huu, siku ile BWANA alipomwokoa mikononi mwa adui zake zote, na mkononi mwa Sauli; akasema, BWANA ndiye jabali langu, na ngome yangu, na mwokozi wangu, naam, wangu; Mungu wa mwamba wangu, nitamwamini yeye; Ngao yangu, na pembe ya wokovu wangu, mnara wangu, na makimbilio yangu; Mwokozi wangu, waniokoa na jeuri. Nitamwita BWANA astahiliye kusifiwa; Hivyo nitaokoka na adui zangu. Maana mawimbi ya mauti yalinizunguka, Mafuriko ya uovu yakanitia hofu. Kamba za kuzimu zilinizunguka; Mitego ya mauti ikanikabili. Katika shida yangu nalimwita BWANA, Naam, nikamlalamikia Mungu wangu
2 Samueli 22:1-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Daudi alimwimbia BWANA maneno ya wimbo huu wakati BWANA alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na pia mkononi mwa Sauli. Akasema: “BWANA ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu, Mungu wangu ni mwamba wangu, ambaye kwake ninakimbilia, ngao yangu na pembe ya wokovu wangu. Yeye ni ngome yangu, kimbilio langu na mwokozi wangu, huniokoa kutoka kwa watu wenye jeuri. Ninamwita BWANA, anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu. “Mawimbi ya mauti yalinizunguka, mafuriko ya maangamizi yalinilemea. Kamba za kuzimu zilinizunguka, mitego ya mauti ilinikabili. Katika shida yangu nalimwita BWANA, nilimlilia Mungu wangu. Kutoka Hekaluni mwake alisikia sauti yangu, kilio changu kikafika masikioni mwake.