2 Samweli 22:1-7
2 Samweli 22:1-7 NEN
Daudi alimwimbia BWANA maneno ya wimbo huu wakati BWANA alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na pia mkononi mwa Sauli. Akasema: “BWANA ni mwamba wangu, ngome yangu na mwokozi wangu, Mungu wangu ni mwamba wangu, ambaye kwake ninakimbilia, ngao yangu na pembe ya wokovu wangu. Yeye ni ngome yangu, kimbilio langu na mwokozi wangu, huniokoa kutoka kwa watu wenye jeuri. Ninamwita BWANA, anayestahili kusifiwa, nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu. “Mawimbi ya mauti yalinizunguka, mafuriko ya maangamizi yalinilemea. Kamba za kuzimu zilinizunguka, mitego ya mauti ilinikabili. Katika shida yangu nalimwita BWANA, nilimlilia Mungu wangu. Kutoka Hekaluni mwake alisikia sauti yangu, kilio changu kikafika masikioni mwake.