Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wimbo Ulio Bora 5:10-16

Wimbo Ulio Bora 5:10-16 BHN

Mpenzi wangu ni mzuri na mwenye nguvu, mashuhuri miongoni mwa wanaume elfu kumi. Kichwa chake kizuri kama dhahabu safi, nywele zake ni za ukoka, nyeusi ti kama kunguru. Macho yake ni kama ya hua kandokando ya kijito, ni kama njiwa waliooga maziwa kando ya kijito. Mashavu yake ni kama matuta ya rihani kama bustani iliyojaa manukato na manemane. Midomo yake ni kama yungiyungi, imelowa manemane kwa wingi. Mikono yake imewekwa bangili za dhahabu, amevalia johari za Tarshishi. Kiwiliwili chake ni kama pembe za ndovu zilizopambwa kwa vito vya johari ya rangi ya samawati. Miguu yake ni kama nguzo za alabasta zilizosimikwa katika misingi ya dhahabu. Umbo lake ni kama Lebanoni, ni bora kama miti ya mierezi. Kinywa chake kimejaa maneno matamu, kwa ujumla anapendeza. Basi, hivyo ndivyo alivyo mpenzi wangu, naam, ndivyo alivyo rafiki yangu, enyi wanawake wa Yerusalemu.