Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Wim 5:10-16

Wim 5:10-16 SUV

Mpendwa wangu ni mweupe, tena mwekundu, Mashuhuri miongoni mwa elfu kumi; Kichwa chake ni kama dhahabu safi sana, Nywele zake ni za ukoka, nyeusi kama kunguru; Macho yake ni kama hua penye vijito, Wakioga kwa maziwa, wakiikalia mito iliyojaa; Mashavu yake ni kama matuta ya rihani, Ambayo hufanyizwa manukato; Midomo yake ni kama nyinyoro, Inadondoza matone ya manemane; Mikono yake ni kama mianzi ya dhahabu, lliyopambwa kwa zabarajadi; Kiwiliwili chake kama kazi ya pembe, Iliyonakishiwa kwa yakuti samawi; Miguu yake ni kama nguzo za marimari, Zilizowekwa juu ya misingi ya dhahabu; Sura yake ni kama Lebanoni, Ni bora mfano wa mierezi; Kinywa chake kimejaa maneno matamu, Ndiye mzuri sana pia pia. Ni huyu mpendwa wangu, ni huyu rafiki yangu, Enyi binti za Yerusalemu.

Soma Wim 5