Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 98:4-9

Zaburi 98:4-9 BHN

Dunia yote imshangilie Mwenyezi-Mungu; imsifu kwa nyimbo na vigelegele. Msifuni Mwenyezi-Mungu kwa shangwe, msifuni kwa sauti tamu za zeze. Mpigieni vigelegele Mwenyezi-Mungu mfalme wetu, mshangilieni kwa tarumbeta na sauti ya baragumu. Bahari na ivume na vyote vilivyomo; dunia na wote waishio ndani yake. Enyi mito pigeni makofi; enyi vilima imbeni pamoja kwa shangwe. Shangilieni mbele ya Mwenyezi-Mungu, maana anakuja kutawala dunia. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, atawatawala watu kwa uadilifu.

Soma Zaburi 98