Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 98:4-9

Zab 98:4-9 SUV

Mshangilieni BWANA, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi. Mwimbieni BWANA zaburi kwa kinubi, Kwa kinubi na sauti ya zaburi. Kwa panda na sauti ya baragumu. Shangilieni mbele za Mfalme, BWANA. Bahari na ivume na vyote viijazavyo, Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake. Mito na ipige makofi, Milima na iimbe pamoja kwa furaha. Mbele za BWANA; Kwa maana anakuja aihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa haki, Na mataifa kwa adili.

Soma Zab 98

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha