Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 98:4-9

Zaburi 98:4-9 SRUV

Mshangilieni BWANA, nchi yote, Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni sifa. Mwimbieni BWANA sifa kwa kinubi, Kwa kinubi na sauti tamu. Kwa panda na sauti ya baragumu. Shangilieni mbele za Mfalme, BWANA. Bahari na ivume na vyote viijazavyo, Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake. Mito na ipige makofi, Milima na iimbe pamoja kwa furaha. Mbele za BWANA; Kwa maana anakuja kuihukumu nchi. Atauhukumu ulimwengu kwa uaminifu, Na mataifa kwa adili.

Soma Zaburi 98