Zaburi 69:13-18
Zaburi 69:13-18 BHN
Lakini mimi nakuomba wewe, ee Mwenyezi-Mungu; nikubalie ombi langu wakati unaopenda, ee Mungu. Kwa wingi wa fadhili zako unijibu. Wewe ni mkombozi wa kuaminika. Kwa msaada wako amini uniokoe nisizame katika matope; uniokoe na hao wanaonichukia, unisalimishe kutoka vilindi vya maji. Usiniache nikumbwe na mkondo wa maji, au nizame kwenye kilindi au nimezwe na kifo. Unijibu, ee Mwenyezi-Mungu, kwa wema na fadhili zako; unielekee kwa wingi wa huruma yako. Usimfiche mtumishi wako uso wako; unijibu haraka, maana niko hatarini. Unijie karibu na kunikomboa, uniokoe na maadui zangu wengi.