Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 69:13-18

Zaburi 69:13-18 SRUV

Nami maombi yangu nakuomba Wewe, BWANA, Wakati ukupendezao; Ee Mungu, Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Katika kweli ya wokovu wako. Uniponye kwa kunitoa matopeni, Wala usiniache nikazama. Na niponywe kutoka kwa wanaonichukia, Na kutoka katika vilindi vya maji. Mkondo usinigharikishe, wala vilindi visinimeze, Wala Shimo lisifumbe kinywa chake juu yangu. Ee BWANA, unijibu, maana fadhili zako ni njema, Kwa kadiri ya rehema zako unielekee. Wala usinifiche uso wako, mimi mtumishi wako, Maana mimi nimo taabuni, unijibu upesi. Uikaribie nafsi yangu, uikomboe, Kwa sababu ya adui zangu unifidie.

Soma Zaburi 69