Zaburi 37:23-27
Zaburi 37:23-27 BHN
Mwenyezi-Mungu huziongoza nyayo za mtu, humlinda yule ampendezaye. Ajapoanguka, haanguki akabaki chini, kwa sababu Mwenyezi-Mungu humtegemeza. Nilikuwa kijana na sasa ni mzee; kamwe sijaona mwadilifu ameachwa na Mungu, au watoto wake wakiombaomba chakula. Daima huwapa wengine kwa furaha na kukopesha, na watoto wake ni baraka. Achana na uovu, utende mema, nawe utaishi nchini daima