Zaburi 3:1-6
Zaburi 3:1-6 BHN
Ee Mwenyezi-Mungu, tazama walivyo wengi adui zangu, ni wengi mno hao wanaonishambulia. Wengi wanasema juu yangu, “Hatapata msaada kwa Mungu.” Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu u ngao yangu kila upande; kwako napata fahari na ushindi wangu. Nakulilia kwa sauti, ee Mungu, nawe wanisikiliza kutoka mlima wako mtakatifu. Nalala na kupata usingizi, naamka tena maana wewe ee Mwenyezi-Mungu wanitegemeza. Sitayaogopa maelfu ya watu, wanaonizingira kila upande.