Zaburi 3:1-6
Zaburi 3:1-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA, watesi wangu wamezidi kuwa wengi, Ni wengi wanaonishambulia, Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu, Hana wokovu huyu kwa Mungu. Na Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu. Kwa sauti yangu namwita BWANA Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu. Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, Kwa kuwa BWANA ananitegemeza. Sitayaogopa makumi elfu ya watu, Waliojipanga juu yangu pande zote.
Zaburi 3:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Ee Mwenyezi-Mungu, tazama walivyo wengi adui zangu, ni wengi mno hao wanaonishambulia. Wengi wanasema juu yangu, “Hatapata msaada kwa Mungu.” Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu u ngao yangu kila upande; kwako napata fahari na ushindi wangu. Nakulilia kwa sauti, ee Mungu, nawe wanisikiliza kutoka mlima wako mtakatifu. Nalala na kupata usingizi, naamka tena maana wewe ee Mwenyezi-Mungu wanitegemeza. Sitayaogopa maelfu ya watu, wanaonizingira kila upande.
Zaburi 3:1-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA, watesi wangu wamezidi kuwa wengi, Ni wengi wanaonishambulia, Ni wengi wanaoiambia nafsi yangu, Hana wokovu huyu kwa Mungu. Lakini Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu. Kwa sauti yangu namwita BWANA Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu. Nilijilaza na kulala usingizi, kisha ninaamka tena, Kwa kuwa BWANA ananitegemeza. Sitayaogopa maelfu na maelfu ya watu, Waliojipanga Juu yangu pande zote.
Zaburi 3:1-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee BWANA, tazama adui zangu walivyo wengi! Ni wengi kiasi gani wanaoinuka dhidi yangu! Wengi wanasema juu yangu, “Mungu hatamwokoa.” Lakini wewe, Ee BWANA, ni ngao pande zote; umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu. Ninamlilia BWANA kwa sauti kuu, naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu. Ninajilaza na kupata usingizi; naamka tena, kwa maana BWANA hunitegemeza. Sitaogopa makumi elfu ya adui, wanaojipanga dhidi yangu kila upande.