Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 136:13-26

Zaburi 136:13-26 BHN

Ndiye aliyeigawa Bahari ya Shamu sehemu mbili; kwa maana fadhili zake zadumu milele, akawapitisha watu wa Israeli humo; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Lakini akawazamisha humo Farao na jeshi lake; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye aliyewaongoza watu wake jangwani; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye aliyewapiga wafalme wenye nguvu; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Akawaua wafalme maarufu; kwa maana fadhili zake zadumu milele; akamuua Sihoni, mfalme wa Waamori, kwa maana fadhili zake zadumu milele; na Ogu, mfalme wa Bashani; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Akachukua nchi zao akawapa watu wake; kwa maana fadhili zake zadumu milele; ziwe riziki ya Israeli, mtumishi wake; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye aliyetukumbuka wakati wa unyonge wetu; kwa maana fadhili zake zadumu milele; akatuokoa kutoka maadui zetu; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye akipaye kila kiumbe chenye uhai chakula; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Mshukuruni Mungu wa mbinguni; kwa maana fadhili zake zadumu milele!

Soma Zaburi 136