Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 136:13-26

Zaburi 136:13-26 SRUV

Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akawavusha Israeli katikati yake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyewapiga wafalme wakuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akawaua wafalme mashuhuri; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Sihoni, mfalme wa Waamori; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Na Ogu, mfalme wa Bashani; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akaitoa nchi yao iwe urithi; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Urithi wa Israeli mtumishi wake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Aliyetukumbuka katika unyonge wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akatuokoa na watesi wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye akipaye kila kiumbe chakula chake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuruni Mungu wa mbingu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Soma Zaburi 136