Zaburi 136:13-26
Zaburi 136:13-26 NEN
Kwake yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele. Na kuwapitisha Israeli katikati yake, Fadhili zake zadumu milele. Lakini alimfagia Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele. Kwake yeye aliyewaongoza watu wake katika jangwa, Fadhili zake zadumu milele. Ambaye aliwapiga wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele. Naye aliwaua wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele. Sihoni mfalme wa Waamori, Fadhili zake zadumu milele. Ogu mfalme wa Bashani, Fadhili zake zadumu milele. Akatoa nchi yao kuwa urithi, Fadhili zake zadumu milele. Urithi kwa Israeli mtumishi wake, Fadhili zake zadumu milele. Aliyetukumbuka katika unyonge wetu, Fadhili zake zadumu milele. Alituweka huru toka adui zetu, Fadhili zake zadumu milele. Ambaye humpa chakula kila kiumbe. Fadhili zake zadumu milele. Mshukuruni Mungu wa mbinguni, Fadhili zake zadumu milele.