Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 129:1-8

Zaburi 129:1-8 BHN

“Nimesumbuliwa vibaya tangu ujana wangu Kila mtu katika Israeli na aseme: “Nimesumbuliwa vibaya tangu ujana wangu, lakini hawakufaulu kunishinda. Walinijeruhi vibaya mgongoni mwangu, wakafanya kama mkulima anayelima shamba. Lakini Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu; amezikata kamba za hao watu waovu.” Na waaibishwe na kurudishwa nyuma, wote wale wanaouchukia mji wa Siyoni. Wawe kama nyasi juu ya paa la nyumba, ambazo hunyauka kabla hazijakua, hakuna anayejishughulisha kuzikusanya, wala kuzichukua kama matita. Hakuna apitaye karibu atakayewaambia: “Mwenyezi-Mungu awabariki! Twawabariki kwa jina la Mwenyezi-Mungu!”

Soma Zaburi 129