Zaburi 129:1-8
Zaburi 129:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)
“Nimesumbuliwa vibaya tangu ujana wangu Kila mtu katika Israeli na aseme: “Nimesumbuliwa vibaya tangu ujana wangu, lakini hawakufaulu kunishinda. Walinijeruhi vibaya mgongoni mwangu, wakafanya kama mkulima anayelima shamba. Lakini Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu; amezikata kamba za hao watu waovu.” Na waaibishwe na kurudishwa nyuma, wote wale wanaouchukia mji wa Siyoni. Wawe kama nyasi juu ya paa la nyumba, ambazo hunyauka kabla hazijakua, hakuna anayejishughulisha kuzikusanya, wala kuzichukua kama matita. Hakuna apitaye karibu atakayewaambia: “Mwenyezi-Mungu awabariki! Twawabariki kwa jina la Mwenyezi-Mungu!”
Zaburi 129:1-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Israeli na aseme sasa, Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Lakini hawakuniweza. Wakulima wamelima mgongoni mwangu, Wamefanya mirefu mifuo yao. BWANA ndiye mwenye haki, Amezikata kamba zao wasio haki. Na waaibishwe, warudishwe nyuma, Wote wanaoichukia Sayuni. Na wawe kama majani ya darini Yanyaukayo kabla hayajamea. Ambayo mvunaji haujazi mkono wake, Wala mfunga miganda kifua chake. Wapitao nao hawasemi, Amani ya BWANA ikae nanyi, Twawabariki kwa jina la BWANA.
Zaburi 129:1-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Israeli na aseme sasa, Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu, Lakini hawakuniweza. Wakulima wamelima mgongoni mwangu, Wamefanya mirefu mifuo yao. BWANA ndiye mwenye haki, Amezikata kamba zao wasio haki. Na waaibishwe, warudishwe nyuma, Wote wanaoichukia Sayuni. Na wawe kama majani ya darini Yanyaukayo kabla hayajamea. Ambayo mvunaji haujazi mkono wake, Wala mfunga miganda kifua chake. Wala hawasemi wapitao, Amani ya BWANA ikae nanyi, Twawabariki kwa jina la BWANA.
Zaburi 129:1-8 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wamenionea mno tangu ujana wangu; Israeli na aseme sasa: wamenionea mno tangu ujana wangu, lakini bado hawajanishinda. Wakulima wamelima mgongo wangu, na kufanya mifereji yao mirefu. Lakini BWANA ni mwenye haki; amenifungua toka kamba za waovu. Wale wote waichukiao Sayuni na warudishwe nyuma kwa aibu. Wawe kama majani juu ya paa, ambayo hunyauka kabla hayajakua; kwa hayo mvunaji hawezi kujaza vitanga vyake, wala akusanyaye kujaza mikono yake. Wale wapitao karibu na wasiseme, “Baraka ya BWANA iwe juu yako; tunakubariki katika jina la BWANA.”