Zaburi 129
129
Sala ya kushindwa kwa adui za Israeli
Wimbo wa Kupanda mlima
1 #
Eze 23:3; Hos 2:15 Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu,
Israeli na aseme sasa,
2Mara nyingi wamenitesa tangu ujana wangu,
Lakini hawakuniweza.
3 #
Ebr 11:36
Wakulima wamelima mgongoni mwangu,
Wamefanya mirefu mifuo yao.
4 #
2 The 1:6
BWANA ndiye mwenye haki,
Amezikata kamba zao wasio haki.
5Na waaibishwe, warudishwe nyuma,
Wote wanaoichukia Sayuni.
6 #
Zab 37:2; Yer 17:5-6 Na wawe kama majani ya darini
Yanyaukayo kabla hayajamea.
7Ambayo mvunaji haujazi mkono wake,
Wala mfunga miganda kifua chake.
8 #
Rut 2:4; Zab 118:26 Wapitao nao hawasemi, Amani ya BWANA ikae nanyi,
Twawabariki kwa jina la BWANA.
Iliyochaguliwa sasa
Zaburi 129: SRUV
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.