Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 118:14-21

Zaburi 118:14-21 BHN

Mwenyezi-Mungu ni nguvu yangu kuu; yeye mwenyewe ndiye wokovu wangu. Sauti za furaha ya ushindi zasikika hemani mwao waadilifu: “Mkono wa Mwenyezi-Mungu umetenda mambo makuu! Mkono wa nguvu wa Mwenyezi-Mungu umeleta ushindi! Mkono wa Mwenyezi-Mungu umetenda mambo makuu!” Sitakufa, bali nitaishi, na kusimulia matendo ya Mwenyezi-Mungu. Mwenyezi-Mungu ameniadhibu sana, lakini hakuniacha nife. Nifungulie milango ya watu waadilifu, niingie na kumshukuru Mwenyezi-Mungu! Huu ndio mlango wa Mwenyezi-Mungu, watu waadilifu watapitia humo. Nakushukuru, ee Mungu kwa kunijibu; kwa sababu wewe ni wokovu wangu.

Soma Zaburi 118