Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 118:14-21

Zaburi 118:14-21 NEN

BWANA ni nguvu yangu na wimbo wangu, yeye amefanyika wokovu wangu. Sauti za shangwe na ushindi zinavuma hemani mwa wenye haki: “Mkono wa kuume wa BWANA umetenda mambo makuu! Mkono wa kuume wa BWANA umeinuliwa juu, mkono wa kuume wa BWANA umetenda mambo makuu!” Sitakufa, bali nitaishi, nami nitatangaza yale BWANA aliyoyatenda. BWANA ameniadhibu vikali, lakini hakuniacha nife. Nifungulie malango ya haki, nami nitaingia na kumshukuru BWANA. Hili ni lango la BWANA ambalo wenye haki wanaweza kuliingia. Nitakushukuru, kwa kuwa ulinijibu, umekuwa wokovu wangu.