Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zab 118:14-21

Zab 118:14-21 SUV

BWANA ni nguvu zangu na wimbo wangu, Naye amekuwa wokovu wangu. Sauti ya furaha na wokovu Imo hemani mwao wenye haki; Mkono wa kuume wa BWANA hutenda makuu. Mkono wa kuume wa BWANA umetukuzwa; Mkono wa kuume wa BWANA hutenda makuu. Sitakufa bali nitaishi, Nami nitayasimulia matendo ya BWANA. BWANA ameniadhibu sana, Lakini hakuniacha nife. Nifungulieni malango ya haki, Nitaingia na kumshukuru BWANA. Lango hili ni la BWANA, Wenye haki ndio watakaoliingia. Nitakushukuru kwa maana umenijibu, Nawe umekuwa wokovu wangu.

Soma Zab 118