Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 104:14-27

Zaburi 104:14-27 BHN

Waotesha nyasi kwa ajili ya mifugo, na mimea kwa matumizi ya binadamu ili naye ajipatie chakula chake ardhini: Divai ya kumchangamsha, mafuta ya zeituni ya kumfurahisha, na mkate wa kumpa nguvu. Miti mikubwa ya Mwenyezi-Mungu yapata maji ya kutosha; naam, mierezi ya Lebanoni aliyoiotesha. Humo, ndege hujenga viota vyao; korongo hufanya maskani yao katika misonobari. Milima mirefu ni makao ya mbuzimwitu; na pelele hupata maficho yao miambani. Umeuumba mwezi utupimie majira; jua nalo lajua wakati wa kutua. Waleta giza, usiku waingia; nao wanyama wote wa porini wanatoka: Wanasimba hunguruma wapate mawindo, humngojea Mungu awape chakula chao. Jua lichomozapo hurudi makwao, na kujipumzisha mapangoni mwao. Hapo naye binadamu huenda kwenye shughuli zake; na kufanya kazi zake mpaka jioni. Ee Mwenyezi-Mungu, umetenda mambo mengi mno! Yote umeyafanya kwa hekima! Dunia imejaa viumbe vyako! Mbali kule iko bahari - kubwa na pana, ambamo kumejaa viumbe visivyohesabika, viumbe hai, vikubwa na vidogo. Ndimo zinamosafiri meli, na lile dude Lewiyathani uliloliumba licheze humo. Wote wanakungojea wewe, uwapatie chakula chao kwa wakati wake.

Soma Zaburi 104