Methali 13:3-7
Methali 13:3-7 BHN
Achungaye mdomo wake huyahifadhi maisha yake, anayeropoka ovyo hujiletea maangamizi. Mvivu hutamani lakini hapati chochote, hali mwenye bidii hujaliwa riziki kwa wingi. Mwadilifu huuchukia uongo, lakini mwovu hutenda kwa aibu na fedheha. Uadilifu huwalinda wenye mwenendo mnyofu, lakini dhambi huwaangusha waovu. Baadhi hujidai kuwa matajiri kumbe hawana kitu; wengine hujiona kuwa maskini hali wana mali tele.