Mithali 13:3-7
Mithali 13:3-7 NENO
Yeye alindaye midomo yake hulinda nafsi yake, bali yeye asemaye kwa haraka ataangamia. Mvivu hutamani sana na hapati kitu, bali nafsi ya mwenye bidii hutoshelezwa kikamilifu. Mwenye haki huchukia uongo, bali waovu huleta aibu na fedheha. Haki humlinda mtu mwadilifu, bali uovu humwangusha mwenye dhambi. Mtu mmoja hujifanya tajiri, kumbe hana chochote; mwingine hujifanya maskini, kumbe ana utajiri mwingi.