Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mathayo 20:17-19

Mathayo 20:17-19 BHN

Yesu alipokuwa anakwenda juu Yerusalemu, aliwachukua wale wanafunzi kumi na wawili faraghani, na njiani akawaambia, “Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu, na huko Mwana wa Mtu atakabidhiwa kwa makuhani wakuu na waalimu wa sheria, nao watamhukumu auawe. Watamkabidhi kwa watu wa mataifa mengine ili adhihakiwe, apigwe viboko na kusulubiwa; lakini siku ya tatu atafufuliwa.”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mathayo 20:17-19