Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 1:39-43

Luka 1:39-43 BHN

Siku kadhaa baadaye, Maria alifunga safari akaenda kwa haraka hadi mji mmoja ulioko katika milima ya Yudea. Huko, aliingia katika nyumba ya Zakaria, akamsalimu Elisabeti. Mara tu Elisabeti aliposikia sauti ya Maria, mtoto mchanga tumboni mwake Elisabeti akaruka. Naye Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu, akasema kwa sauti kubwa, “Umebarikiwa kuliko wanawake wote, naye utakayemzaa amebarikiwa. Mimi ni nani hata mama wa Bwana wangu afike kwangu?

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Luka 1:39-43