Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 1:39-43

Luka 1:39-43 SRUV

Basi, Mariamu akaondoka siku hizo, akaenda hadi katika nchi yenye milima kwa haraka mpaka mji mmoja wa Yudea, akaingia nyumbani kwa Zakaria akamwamkia Elisabeti. Ikawa Elisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake; Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu; akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijie mimi?

Soma Luka 1

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Luka 1:39-43