Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yoshua 21:43-45

Yoshua 21:43-45 BHN

Basi, Mwenyezi-Mungu aliwapa Waisraeli nchi yote ambayo alikuwa amewaahidi wazee wao. Nao wakaimiliki na kuishi humo. Mwenyezi-Mungu akawapa amani kila mahali nchini kama alivyowaapia wazee wao. Hakuna adui yeyote aliyethubutu kuwakabili kwani Mwenyezi-Mungu alikuwa amewatia adui hao mikononi mwao. Hakuna hata ahadi yoyote njema ambayo Mwenyezi-Mungu aliiahidi Israeli ambayo haikutimia. Ahadi zote zilitimia.

Soma Yoshua 21