Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yoshua 21:43-45

Yoshua 21:43-45 NEN

Kwa hiyo BWANA akawapa Israeli nchi yote aliyokuwa ameapa kuwapa baba zao, nao wakaimiliki na kukaa humo. BWANA akawapa pumziko kila upande, kama vile alivyokuwa amewaapia baba zao, hakuna hata mmoja wa adui zao aliyeweza kusimama mbele yao, BWANA akawatia adui zao wote mikononi mwao. Hakuna hata mojawapo ya ahadi nzuri ya BWANA kwa nyumba ya Israeli ambayo haikutimia; kila moja ilitimia.