Yobu 38:1-7
Yobu 38:1-7 BHN
Hapo Mwenyezi-Mungu alimjibu Yobu kutoka dhoruba: “Nani wewe unayevuruga mashauri yangu kwa maneno yasiyo na akili? Jikaze kama mwanamume, nami nitakuuliza nawe utanijibu. “Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya dunia? Niambie, kama una maarifa. Ni nani aliyeweka vipimo vyake, wajua bila shaka! Au nani aliyelaza kamba juu yake kuipima? Je, nguzo za dunia zimesimikwa juu ya nini, au nani aliyeliweka jiwe lake la msingi, nyota za asubuhi zilipokuwa zikiimba pamoja, na wana wa Mungu wakapaza sauti za shangwe?