Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayu 38:1-7

Ayu 38:1-7 SUV

Ndipo BWANA akamjibu Ayubu katika upepo wa kisulisuli, na kusema, Ni nani huyu atiaye mashauri giza Kwa maneno yasiyo na maarifa? Basi jifunge viuno kama mwanamume, Maana nitakuuliza neno, nawe niambie. Ulikuwa wapi nilipoiweka misingi ya nchi? Haya! Sema, kama ukiwa na ufahamu. Ni nani aliyeamrisha vipimo vyake, kama ukijua? Au ni nani aliyenyosha kamba juu yake? Misingi yake ilikazwa juu ya kitu gani? Au ni nani aliyeliweka jiwe lake la pembeni, Hapo nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, Na wana wote wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha?

Soma Ayu 38

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Ayu 38:1-7