Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yobu 27:1-12

Yobu 27:1-12 BHN

Yobu akaendelea kutoa hoja yake, akasema: “Naapa kwa Mungu aliye hai, aliyeniondolea haki yangu, Mungu Mwenye Nguvu aliyeifanya nafsi yangu iwe na uchungu! Naapa kuwa kadiri ninavyoweza kupumua, roho ya Mungu ikiwa bado ndani yangu; midomo yangu kamwe haitatamka uongo, wala ulimi wangu kusema udanganyifu. Siwezi kabisa kusema kuwa nyinyi mnasema ukweli mpaka kufa kwangu nasema sina hatia. Nashikilia unyofu wangu, wala sitauacha; katika dhamiri yangu sina cha kunihukumu maishani mwangu. “Adui yangu na apate adhabu ya mwovu, anayeinuka kunilaumu aadhibiwe kama mbaya. Asiyemcha Mungu ana tumaini gani, Mungu anapomkatilia mbali, anapomwondolea uhai wake? Je, atakapokumbwa na taabu, Mungu atasikia kilio chake? Mwovu hawezi kufurahi mbele ya Mungu Mwenye Nguvu; hataweza kudumu akimwomba Mungu. Nitawafundisheni kitendo cha Mungu kilivyo, sitawaficheni mipango yake Mungu Mwenye Nguvu. Lakini nyinyi mnajua jambo hilo vizuri sana! Mbona, basi mnaongea upuuzi?

Soma Yobu 27