Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yobu 25:1-6

Yobu 25:1-6 BHN

Kisha Bildadi, Mshuhi, akajibu: “Mungu ni mwenye uwezo mkuu, watu wote na wamche. Yeye huweka amani mpaka juu kwake mbinguni. Nani awezaye kuhesabu majeshi yake? Ni nani asiyeangaziwa na mwanga wake? Mtu awezaje basi, kuwa mwadilifu mbele ya Mungu? Binadamu tu awezaje kujidai kuwa safi? Kwake Mungu, hata mwezi haungai vya kutosha; nyota nazo si safi mbele yake; sembuse mtu ambaye ni mdudu, binadamu ambaye ni buu tu!”

Soma Yobu 25