Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 25:1-6

Ayubu 25:1-6 SRUV

Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema, Enzi na hofu zi pamoja na Mungu; Hufanya amani katika mahali pake palipoinuka. Je! Majeshi yake yahesabika? Ni nani asiyetokewa na mwanga wake? Basi mtu awezaje kuwa na haki mbele ya Mungu? Au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke? Tazama, hata mwezi hauangazi, Wala nyota si safi machoni pake; Seuze mtu, aliye mdudu! Na mwanadamu, ambaye ni buu!

Soma Ayubu 25