Ayubu 25:1-6
Ayubu 25:1-6 NEN
Ndipo Bildadi Mshuhi akajibu: “Mamlaka na kuheshimiwa ni vyake Mungu; yeye huthibitisha amani katika mbingu juu. Je, majeshi yake yaweza kuhesabika? Ni nani asiyeangaziwa na nuru yake? Mtu awezaje kuwa mwadilifu mbele za Mungu? Awezaje mtu aliyezaliwa na mwanamke kuwa safi? Ikiwa hata mwezi sio mwangavu nazo nyota si safi machoni pake, sembuse mtu ambaye ni funza: mwanadamu ambaye ni buu tu!”