Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia 25:32-38

Yeremia 25:32-38 BHN

Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema: “Tazama, maafa yatalikumba taifa moja baada ya lingine, na tufani itazuka kutoka miisho ya dunia.” Siku hiyo, watakaouawa na Mwenyezi-Mungu watatapakaa kutoka upande mmoja wa dunia hadi mwingine. Hawataombolezewa, hawatakusanywa wala kuzikwa; watabaki kuwa mavi juu ya ardhi. Ombolezeni enyi wachungaji; lieni na kugaagaa majivuni enyi wakuu wa kundi; siku za kuchinjwa kwenu na kutawanywa zimefika; mtauawa kama kondoo madume waliochaguliwa. Wachungaji hawatakuwa na pa kukimbilia, wala wakuu wa kundi hawataweza kutoroka. Sikilizeni kilio cha wachungaji na mayowe ya wakuu wa kundi! Mwenyezi-Mungu anayaharibu malisho yao, na makundi yaliyokuwa matulivu yameharibiwa kwa sababu ya hasira kali ya Mwenyezi-Mungu. Mwenyezi-Mungu amewaacha watu wake, kama vile simba aachavyo pango lake; nchi yao imekuwa jangwa tupu, kwa sababu ya vita vya wadhalimu, na hasira kali ya Mwenyezi-Mungu.

Soma Yeremia 25

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha