Yeremia 25:32-38
Yeremia 25:32-38 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hili ndilo BWANA Mwenye Nguvu Zote asemalo: “Tazama! Maafa yanaenea kutoka taifa moja hadi jingine; tufani kubwa inainuka kutoka miisho ya dunia.” Wakati huo, hao waliouawa na BWANA watatapakaa kila mahali, kuanzia mwisho mmoja wa dunia hadi mwisho mwingine. Hawataombolezewa wala kukusanywa au kuzikwa, lakini watakuwa kama mavi yaliyoenea juu ya ardhi. Lieni na kuomboleza, enyi wachungaji, mgaagae mavumbini, ninyi viongozi wa kundi. Kwa maana wakati wenu wa kuchinjwa umewadia; mtaanguka na kuvunjavunjwa kama vyombo vizuri vya udongo. Wachungaji hawatakuwa na mahali pa kukimbilia, viongozi wa kundi hawatapata mahali pa kutorokea. Sikia kilio cha wachungaji, maombolezo ya viongozi wa kundi, kwa maana BWANA anayaharibu malisho yao. Makao yao ya amani yataharibiwa kwa sababu ya hasira kali ya BWANA. Kama simba ataacha pango lake, nchi yao itakuwa ukiwa kwa sababu ya upanga wa mdhalimu, na kwa sababu ya hasira kali ya BWANA Mungu.
Yeremia 25:32-38 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema: “Tazama, maafa yatalikumba taifa moja baada ya lingine, na tufani itazuka kutoka miisho ya dunia.” Siku hiyo, watakaouawa na Mwenyezi-Mungu watatapakaa kutoka upande mmoja wa dunia hadi mwingine. Hawataombolezewa, hawatakusanywa wala kuzikwa; watabaki kuwa mavi juu ya ardhi. Ombolezeni enyi wachungaji; lieni na kugaagaa majivuni enyi wakuu wa kundi; siku za kuchinjwa kwenu na kutawanywa zimefika; mtauawa kama kondoo madume waliochaguliwa. Wachungaji hawatakuwa na pa kukimbilia, wala wakuu wa kundi hawataweza kutoroka. Sikilizeni kilio cha wachungaji na mayowe ya wakuu wa kundi! Mwenyezi-Mungu anayaharibu malisho yao, na makundi yaliyokuwa matulivu yameharibiwa kwa sababu ya hasira kali ya Mwenyezi-Mungu. Mwenyezi-Mungu amewaacha watu wake, kama vile simba aachavyo pango lake; nchi yao imekuwa jangwa tupu, kwa sababu ya vita vya wadhalimu, na hasira kali ya Mwenyezi-Mungu.
Yeremia 25:32-38 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, uovu utatokea toka taifa hata taifa, na tufani kuu itainuliwa toka pande za mwisho wa dunia. Na waliouawa na BWANA siku ile watakuwapo, toka upande mmoja wa dunia hata upande wa pili; hawataliliwa, wala kukusanywa, wala kuzikwa; watakuwa samadi juu ya uso wa nchi. Ombolezeni, enyi wachungaji, na kulia; na kugaagaa katika majivu, enyi mlio hodari katika kundi; maana siku za kuuawa kwenu zimetimia kabisa, nami nitawavunja vipande vipande, nanyi mtaanguka kama chombo cha anasa. Nao wachungaji watakuwa hawana njia ya kukimbia, wala walio hodari katika kundi hawataokoka. Sauti ya kilio cha wachungaji, na sauti ya kuomboleza kwao walio hodari katika kundi, kwa maana BWANA anayaharibu malisho yao. Na mazizi yenye amani yamenyamazishwa, kwa sababu ya hasira kali ya BWANA. Ameacha mahali pake pa kujificha, kama simba; maana nchi yao imekuwa kitu cha kushangaza, kwa sababu ya ukali wa upanga uoneao, na kwa sababu ya hasira yake kali.
Yeremia 25:32-38 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA wa majeshi asema hivi, Tazama, uovu utatokea toka taifa hata taifa, na tufani kuu itainuliwa toka pande za mwisho wa dunia. Na waliouawa na BWANA siku ile watakuwapo, toka upande mmoja wa dunia hata upande wa pili; hawataliliwa, wala kukusanywa, wala kuzikwa; watakuwa samadi juu ya uso wa nchi. Pigeni yowe, enyi wachungaji, na kulia; na kugaagaa katika majivu, enyi mlio hodari katika kundi; maana siku za kuuawa kwenu zimetimia kabisa, nami nitawavunja vipande vipande, nanyi mtaanguka kama chombo cha anasa. Nao wachungaji watakuwa hawana njia ya kukimbia, wala walio hodari katika kundi hawataokoka. Sauti ya kilio cha wachungaji, na sauti ya kupiga yowe kwao walio hodari katika kundi, kwa maana BWANA anayaharibu malisho yao. Na mazizi yenye amani yamenyamazishwa, kwa sababu ya hasira kali ya BWANA. Ameacha mahali pake pa kujificha, kama simba; maana nchi yao imekuwa kitu cha kushangaza, kwa sababu ya ukali wa upanga uoneao, na kwa sababu ya hasira yake kali.