Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia 12:1-4

Yeremia 12:1-4 BHN

Ee Mwenyezi-Mungu, wewe ni mwadilifu, ingawa nakulalamikia. Lakini ningependa kutoa hoja zangu mbele yako: Kwa nini waovu hufanikiwa katika mambo yao? Mbona wote wenye hila hustawi? Unawaotesha nao wanaota; wanakua na kuzaa matunda. Wanakutaja kwa maneno yao, lakini mioyo yao iko mbali nawe. Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu wanijua; wayathibiti maelekeo yangu kwako. Uwaokote hao kama kondoo wa kuchinjwa, watenge kwa ajili ya wakati wa kuuawa. Mpaka lini nchi itaomboleza kwa ukame, na nyasi za mashamba yote kunyauka? Wanyama na ndege wanakufa kwa uovu wa wakazi wake; wanasema: “Mungu hataona mwisho wetu.”

Soma Yeremia 12