Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia 12:1-4

Yeremia 12:1-4 NEN

Wewe daima u mwenye haki, Ee BWANA, niletapo mashtaka mbele yako. Hata hivyo nitazungumza nawe kuhusu hukumu yako: Kwa nini njia ya waovu inafanikiwa? Kwa nini wasio waaminifu wote wanaishi kwa raha? Umewapanda, nao wameota, wanakua na kuzaa matunda. Daima u midomoni mwao, lakini mbali na mioyo yao. Hata hivyo unanijua mimi, Ee BWANA; unaniona na kuyachunguza mawazo yangu kukuhusu wewe. Wakokote kama kondoo wanaokwenda kuchinjwa! Watenge kwa ajili ya siku ya kuchinjwa! Je, nchi itakaa katika hali ya kuomboleza mpaka lini, na majani katika kila shamba kunyauka? Kwa sababu wale waishio ndani yake ni waovu, wanyama na ndege wameangamia. Zaidi ya hayo, watu wanasema, “BWANA hataona yatakayotupata sisi.”