Isaya 43:25-28
Isaya 43:25-28 BHN
Walakini mimi ndimi niliyefuta makosa yenu kwa heshima yangu, ndimi niyafutaye makosa kwa ajili yangu mwenyewe, na wala sitazikumbuka dhambi zenu. “Niambie kama mna kisa nami, njoo tukahojiane; toeni mashtaka yenu ili tuuone ukweli wenu! Babu yenu wa kwanza alitenda dhambi, wapatanishi wenu waliniasi. Kwa hiyo niliwafanya haramu wakuu wa mahali patakatifu nikawaacha watu wa Yakobo waangamizwe, naam, nikawaacha Waisraeli watukanwe.”