Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 43:25-28

Isaya 43:25-28 NEN

“Mimi, naam mimi, ndimi nizifutaye dhambi zako, kwa ajili yangu mwenyewe, wala sizikumbuki dhambi zako tena. Tafakari mambo yaliyopita, njoo na tuhojiane, leta shauri lako uweze kupewa haki yako. Baba yako wa kwanza alitenda dhambi, wasemaji wako wameasi dhidi yangu. Kwa hiyo nitawaaibisha wakuu wa Hekalu lako, nami nitamtoa Yakobo aangamizwe, na Israeli adhihakiwe.