Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 49:1-13

Mwanzo 49:1-13 BHN

Yakobo akawaita wanawe, akasema, “Kusanyikeni pamoja niwaambieni mambo yatakayowapata siku zijazo. “Kusanyikeni msikie, enyi wana wa Yakobo, nisikilizeni mimi Israeli, baba yenu. “Wewe Reubeni ni mzaliwa wangu wa kwanza, nguvu yangu na tunda la ujana wangu. Wewe wawapita ndugu zako kwa ukuu na nguvu. “Wewe ni kama maji ya mafuriko. Lakini hutakuwa wa kwanza tena, maana ulipanda kitandani mwangu mimi baba yako, wewe ulikitia najisi; naam wewe ulikipanda! “Simeoni na Lawi ni ndugu: Silaha zao wanatumia kufanya ukatili, lakini mimi sitashiriki njama zao; ee roho yangu, usishiriki mikutano yao, maana, katika hasira yao, walimuua mtu, kwa utundu wao walikata mshipa wa ng'ombe. “Nalaani hasira yao maana ni kali mno, na ghadhabu yao isiyo na huruma. Nitawatawanya katika nchi ya Yakobo, nitawasambaza katika nchi ya Israeli. “Wewe Yuda, ndugu zako watakusifu. Adui zako utawakaba shingo; na ndugu zako watainama mbele yako. “Wewe Yuda, mwanangu, ni kama mwanasimba ambaye amepata mawindo yake akapanda juu. Kama simba hujinyosha na kulala chini; simba mwenye nguvu, nani athubutuye kumwamsha? “Fimbo ya kifalme haitatoka kwa Yuda, wala bakora ya utawala miguuni pake, mpaka atakapofika yule ambaye ni yake; ambaye mataifa yatamtii. “Atafunga punda wake katika mzabibu na mwanapunda wake kwenye mzabibu bora. Hufua nguo zake katika divai, na mavazi yake katika divai nyekundu. “Macho yake ni mekundu kwa divai, meno yake ni meupe kwa maziwa. “Zebuluni ataishi sehemu za pwani, pwani yake itakuwa mahali pa kuegesha meli. Nchi yake itapakana na Sidoni.

Soma Mwanzo 49