Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezekieli 40:48-49

Ezekieli 40:48-49 BHN

Baadaye, alinipeleka kwenye ukumbi wa kuingilia nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Akalipima lango, nalo lilikuwa na kimo cha mita 2.5 na upana wa mita 7. Na kuta zake zilikuwa na unene mita 1.5 kila upande. Kulikuwa na ngazi za kupandia kwenye ukumbi wa chumba cha kuingilia, ambao ulikuwa na upana wa mita 10 na kina cha mita 6. Kulikuwa na nguzo mbili, nguzo moja kila upande wa mlango.