Ezekieli 40:48-49
Ezekieli 40:48-49 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo akanileta mpaka ukumbi wa nyumba, akapima kila mwimo wa ukumbi, dhiraa tano upande huu, na dhiraa tano upande huu; na upana wa lango ulikuwa dhiraa tatu upande huu, na dhiraa tatu upande huu. Urefu wa ukumbi ulikuwa dhiraa ishirini, na upana wake dhiraa kumi na moja; karibu na madaraja ambayo waliupandia; tena palikuwa na nguzo karibu na miimo, moja upande huu, na moja upande huu.
Ezekieli 40:48-49 Biblia Habari Njema (BHN)
Baadaye, alinipeleka kwenye ukumbi wa kuingilia nyumba ya Mwenyezi-Mungu. Akalipima lango, nalo lilikuwa na kimo cha mita 2.5 na upana wa mita 7. Na kuta zake zilikuwa na unene mita 1.5 kila upande. Kulikuwa na ngazi za kupandia kwenye ukumbi wa chumba cha kuingilia, ambao ulikuwa na upana wa mita 10 na kina cha mita 6. Kulikuwa na nguzo mbili, nguzo moja kila upande wa mlango.
Ezekieli 40:48-49 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo akanileta mpaka ukumbi wa nyumba, akapima kila mwimo wa ukumbi, dhiraa tano upande huu, na dhiraa tano upande huu; na upana wa lango ulikuwa dhiraa tatu upande huu, na dhiraa tatu upande huu. Urefu wa ukumbi ulikuwa dhiraa ishirini, na upana wake dhiraa kumi na moja; karibu na madaraja ambayo waliupandia; tena palikuwa na nguzo karibu na miimo, moja upande huu, na moja upande huu.
Ezekieli 40:48-49 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Akanileta mpaka kwenye baraza ya Hekalu naye akaipima miimo ya hiyo baraza, nayo ilikuwa na upana wa dhiraa tatu kila upande. Upana wa ingilio ulikuwa dhiraa kumi na nne na kuta zake zilikuwa na upana wa dhiraa tatu kila upande. Baraza ilikuwa na dhiraa ishirini kwenda juu na dhiraa kumi na mbili kuanzia mbele hadi nyuma. Kulikuwa na ngazi kumi za kupandia huko, pia kulikuwa na nguzo kwa kila upande wa miimo.