Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ezekieli 40:48-49

Ezekieli 40:48-49 NEN

Akanileta mpaka kwenye baraza ya Hekalu naye akaipima miimo ya hiyo baraza, nayo ilikuwa na upana wa dhiraa tatu kila upande. Upana wa ingilio ulikuwa dhiraa kumi na nne na kuta zake zilikuwa na upana wa dhiraa tatu kila upande. Baraza ilikuwa na dhiraa ishirini kwenda juu na dhiraa kumi na mbili kuanzia mbele hadi nyuma. Kulikuwa na ngazi kumi za kupandia huko, pia kulikuwa na nguzo kwa kila upande wa miimo.